Guterres atoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Gaza

Tom Mathinji
1 Min Read
Wanajeshi wa Israel wazidisha mashambulizi Gaza.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza wito wake wa kusitisha mapigano mara moja Gaza, na kuachiliwa kwa mateka waliotekwa na Hamas.

Matamshi ya Guterres yanajiri huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akitangaza kuwa Israel imeingia katika hatua ya pili ya vita vyake na Hamas

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Nepal, Guterres alirudia ombi lake la kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu, kuachiliwa bila masharti kwa mateka wote, na utoaji wa misaada endelevu ya kibinadamu kwa kiwango ambacho kinakidhi mahitaji ya watu wa Gaza.

Aidha katibu huyo mkuu alilaani mashambulizi ya kutisha yaliyofanywa na Hamas tarehe saba mwezi Oktoba, na kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wanafunzi kumi wa Nepal waliouawa katika shambulio hilo.

Guterres alisema anatumai kurejea salama kwa mtu ambaye bado hajapatikana.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Israel imeweka wanajeshi na makamanda katika Ukanda wa Gaza.

Website |  + posts
Share This Article