Guinea kuandaa uchaguzi wa Urais Disemba 28 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021

Dismas Otuke
0 Min Read

Guinea itaandaa uchaguzi mkuu wa urais kwa mara ya kwanza Disemba 28 mwaka huu, ikiwa mara ya kwanza tangu mapinduzi ya serikali mwaka 2021.

Tangazo hilo lilitolewa Jumamosi iliyopita, siku moja baada ya Mahakama ya Upeo kuhalalisha matokeo ya kura ya maoni inayoruhusu mabadiliko ya katiba.

Guinea ni mojawapo ya mataifa ya Afrika Magharibi yaliyoathirika pakubwa na mapinduzi ya serikali, ikiwemo Chad na Gabon.

 

Website |  + posts
Share This Article