Kocha wa Machester City Pep Guardiola amekiri kwamba ameshangazwa na uwezo wa Erling Haaland wa kufunga mabao huku timu hiyo ikijiandaa kuanza kampeni ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Inter Milan.
Mchuano kati ya timu hizo mbili utasakatwa leo Jumatano usiku.
Haaland aliyesajiliwa kutoka Borussia Dortmund mwaka 2022, ameanza vyema msimu wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza huku akiwa amefunga mabao tisa katika mechi nne.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atafikisha idadi ya mabao 100 iwapo atafunga leo usiku kwani anajivunia mabao 99 katika mechi 103.
Aidha, Guardiola aliisifu Inter Milan walioishinda kwenye fainali ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya mwaka 2023.