Gravity Omutujju asema Cindy hahitajiki kwenye shirikisho jipya la wanamuziki

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki wa mtindo wa Rap nchini Uganda Gravity Omutujju anaamini kwamba rais wa muungano wa wanamuziki nchini humo UMA Cinderella Sanyu maarufu kama Cindy hana jukumu la kutekeleza kwenye shirikisho la wanamuziki nchini humo yaani, “Uganda National Musician Federation ( UNMF)”.

Gravity anahisi kwamba Cindy hatakii mwasisi wa shirikisho hilo jipya Eddy Kenzo mazuri kwani hana sababu ya kutojiunga nalo. Anasema Cindy alipatiwa mwaliko wa kujiunga na shirikisho hilo lakini akakataa.

“Hatakii tasnia ya muziki mazuri. Hataki Kenzo afanikiwe.” alisema Omutujju kwenye mahojiano na jukwaa fulani la mitandaoni. Alisema kwamba wanaopinga uongozi wa Kenzo hawataki umoja wa wanamuziki nchini Uganda.

Kenzo alitangaza kubuniwa kwa shirikisho hilo kwa jina “Uganda National Musicians Federation (UNMF)” Mei, 2023 ambapo pia alitoa orodha ya viongozi. Mlezi wa shirikisho hilo ni waziri mkuu Bi. Robinah Nabbanja, huku Eddy Kenzo akiwa rais.

Manaibu wa Kenzo ni watatu ambao ni Shebah Karungi, Pallaso na Juliana Kanyomozi. Shirikisho hilo limeamua kutumia viongozi wa sasa wa muungano wa wanamuziki nchini humo – UMA wa maeneo mbali mbali kuratibu shughuli zao nyanjani.

Bi. Nabbanja alitoa ahadi ya kupigania haki za wanamuziki akisema kwamba serikali itawekeza pakubwa kwenye shirikisho hilo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *