Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya FKF,Gor Mahia wametoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Nzoia Sugar .
Barisa Mohamed alipachika magoli yote mawili kwa Nzoia kunako dakika ya 9 na 30, kabla ya Patrick kaddu kukomboa moja kwa Sirkal kabla ya mapumziko.
Benson Omalla alisawazisha dakika ya 59 kupitia penati huku Gor wakinusuru alama moja katika uwanja wa Homabay.
Ulinzi Stars wakicheza ugenini dhidi ya Muranga Seal, wamelazimisha sare ya goli moja kwa moja Mark Bikokwa akifungua ukurasa kwa wanajeshi dakika ya 31, kabla ya Batts Awita kukomboa dakika ya 77.
Kenya Commercial Bank wametoka sare kappa dhidi ya Talanta FC huku Nairobi City Stars wakihitaji bao la dakika ya nne lililofungwa na Robinson Asenwa kusajili ushindi dhidi ya Bandari FC.