Gor Mahia,KCB washinda mechi za Ligi Kuu

Kenta Commerrcial Bank pia walipata ushindi uo huo wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Mathare United katika kiwara cha Police Sacco.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Gor Mahia walisajili ushindi wa bao moja kwa bila ugenini katika uwanja wa Raila Odinga, kaunti ya Homa Bay dhidi ya wenyeji APS Bomet .

Mechi hiyo ya ligi kuu ya Sportpesa ilishuhudia Alpha Onyango aliwafungia Gor bao pekee  kunako dakika ya 84.

The Green Army wamezoa alama zote sita kutokana na mechi mbili huku APS waliendelea kusubiri ushindi wa kwanza baada ya kwenda sarea na Mathare United katika mechi ya kufungua msimu.

Kenta Commerrcial Bank pia walipata ushindi uo huo wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Mathare United katika kiwara cha Police sacco.

Nguvu mpya Assis Mambote alifunga bao la wahifadhi hela KCB.

Share This Article