Gor Mahia walitemwa nje ya kipute cha ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi usiku kufuatia kipigo cha mabao matatu kwa bila na wenyeji Al Ahly SC ya Misri mjini Cairo.
Rabia Rami alipachika la kwanza dakika ya 23 kabla ya Ali Abou na Taher Mohammed kuongeza la pili na tatu kunako dakika za 50 na 91 mtawalia.
Gor ambao ni mabingwa wa Kigi Kuu ya Kenya waliyaaga mashindano hayo kwa jumla ya yshibde wa magoli sita bila jibu, baada ya kupigwa nyumbani Nairobi tatu bila wiki jana katika duru ya kwanza mchujo wa pili.
Ahly ambo ni mabingwa watetezi wametimu raundi ya kufuati ushindi huo.