Mabingwa wa Ligi Kuu Kenya,Gor Mahia walianza vibaya mashindano ya kombe la CECAFA kwa kichapo cha bao moja bila jibu , kutoka kwa mabingwa wa Zambia ,Red Arrows.
Mechi hiyo iliyosakatwa kiwarani Azam Complex jijini Dar es Salaam Tanzania iliishia sare tasa kunako kipindi cha kwanza, kabla ya Arrows kujipatia bao la pekee la ushindi dakika ya 73 kupitia kwa James Chamanga .
Gor almaarufu Sir Kal watarejea uwanjani Jumamosi hii kwa mchuano wa pili wa kundi B dhidi Djibouti Telecoms.
Al Hilal ya Sudan iliwakomoa Djibouti Telecoms mabao mawili kwa nunge katika mchuano wa kwanza kundi B Jumatano jioni.