Mabingwa watetezi Gor Mahia, watatuzwa taji la 21 Jumapili hii baada ya kumenyana na Bidco United ugani Kenyatta kwenye mechi ya 34 na ya mwisho wa msimu.
Kwa sasa Gor Mahia inaongoza jedwali kwa alama 70, alama nane mbele ya Tusker FC inayoshikilia nafasi ya pili.
Kufuatia ushindi huo, wataiwakilisha kenya kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika CAF.
Mechi nyingine za KPL zimeratibiwa kusakatwa sehemu mbalimbali za taifa.
Kule muhoroni huenda Poster Rangers wakajipata pabaya kwani mwenyeji ana mpango wa kuhepa kushushwa daraja hasa kutokana na kichapo cha magoli sita kwa yai alichoipa Nzoia Sugar.
Jijini Nairobi, Murang’a SEAL watawaalika shabana uwanjani Sportspesa wakati Tuskwer walio maliza wa pili wakiwakaribisha Kakamega Homeboyz pale Ruaraka.
Wanajeshi (Ulinzi) watafwatua risasi ya mwisho dhidi ya chui (AFC Leoparsds) nyumbani (Ulinzi Sports complex) huku wanabunduki wenza-Police wakiwalenga Kariobangi Sharks ugani Police sacco.
Mashabiki wa Talanta na Bandari wataenda Kasarani kushabikia timu zao huku wale wa KCB na City Stars wakijimwaya ndani ya uga wa utalii. Katika uwanja wa Dandora, Batoto ba Mung (Sofapaka) watawaalika Nzoia Sugar wanaoburura mkia.
Mechi zote zitaanza saa tisa alasiri.