Mabingwa wa Kenya Gor Mahia watachuana na El Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini katika mchujo wa kwanza kuwania taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchuano huo utaandaliwa mjini Juba Sudan Kusini siku ya Jumapili huku marudio yakiandaliwa ugani Nyayo wikendi ijayo.
Mshindi wa mechi hiyo baada ya mikondo miwili atafuzu kwa raundi ya pili .
K’ogalo wanarejea mashindanoni baada ya kutimuliwa mwaka jana kwa kukiuka sheria za usajili wachezaji.