Klabu ya Gor Mahia itacheza mechi zake za ligi ya mabingwa msimu ujao nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Sam Ochola, watalazimika kutafuta viwanja vya kuchezea mechi za nyumbani baada ya Shirikisho la Kandanda Afrika, CAF kudinda kujumuisha nyuga za Kasarani na Nyayo katika orodha ya viwanja vilivyoafiki viwango vya kuchezea mechi hizo.
Ochola ameongeza kuwa tayari wamebaini viwanja hivyo ambavyo ni Azam Sports Complex kwa mechi za mchujo na Benjamin Mkapa ikiwa watafuzu kwa hatua ya makundi.
Tanzania ndio pekee kati ya mataifa ya Afrika Mashariki iliyo na viwanja vilivyoidhinishwa na CAF kwa mechi za kimataifa.
Kenya, Uganda na Tanzania zimetuma ombi la pamoja kuandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027.