Gigy Money afungulia umma maisha yake

Marion Bosire
1 Min Read
Gigy Money

Mwanamuziki wa Tanzania Gigy Money ameamua kufungulia umma maisha yake kupitia kwa onyesho la matukio halisi kumhusu kwenye runinga ya Zamaradi.

Onyesho hilo lilizinduliwa rasmi Mei 2, 2024 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambapo yeye na watu wa familia yake walifika wakiwa wamevaa nadhifu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gigy alifichua alipoafikia jina lake la usanii ambapo alisema kwamba la kwanza “Gigy” linatokana na jina lake halisi “Gift” na la pili “Money” ni pesa ambazo aliambiwa babake mzazi alikuwa nazo hata ingawa hakuwahi kukutana naye.

Kuhusu kutumiwa na wengi kupata umaarufu mitandaoni, Gigy alisema hawezi kuelezea mvuto alionao mitandaoni lakini anajua ni Mungu amemchagua.

Watakaongaziwa kwenye kipindi hicho ni pamoja na mamake Gigy kwa jina Lisa, dada zake wawili Jasmine na Veronica, binti take Myra na wapwa zake akiwemo Alicia.

Mmiliki wa Zamaradi TV kwa jina Zamaradi Mketema anasema aliamua kumpa Gigy fursa hiyo kwa sababu anahisi kwamba maisha yake yanastahili kuangaziwa huku akipata hela.

Runinga ya Zamaradi ina vipindi vya matukio halisi kuhusu maisha ya kila siku ya watu maarufu kama vile mtangazaji wa redio Diva kati ya wengine wengine.

Zamaradi Tv huangazia sana burudani na mitindo ya maisha katika vipindi vyake.

Share This Article