Gideon Moi agura kinyang’anyiro cha Useneta Baringo

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi.

Mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi, amejiondoa kwenye uwaniaji wa kiti cha Useneta cha Baringo katika uchaguzi mdogo ujao mwezi Novemba 27, 2025.

Kulingana na Katibu Mkuu wa KANU George Wainaina, chama hicho hakitakuwa na mwaniaji kwenye uchaguzi huo mdogo, na hivyo kumwacha mwaniaji wa chama cha UDA Kiprono Cheburet Chemitei kujipima nguvu na wawaniaji wengine watano.

Hatua hiyo inajiri baada ya msafara wa Chemitei kushambuliwa Alhamisi asubuhi mjini Kabarnet, huku akitoroka eneo hilo kutumia helikopta ili kuwasilisha vyeti vyake vya uteuzi kwa afisi wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka IEBC.

Wadhifa wa Seneta wa Baringo uliachwa wazi kufuatia kifo cha Seneta William Cheptumo mnamo Februari 16, 2025.

Website |  + posts
Share This Article