Seneta wa zamani wa Baringo Gideon Moi ametakiwa kufika mbele ya Bunge la Kitaifa kujibu maswali kuhusu kipande cha ardhi cha ekari 5,000 cha chuo cha Rift Valley Institute of Science and Technology (RVIST).
Moi pia atajibu maswali kuhusu ardhi nyingine ya ekari 200 za thamani ya shilingi bilioni 1.08, ambayo taasisi hiyo imejengwa.
Moi atafika mbele ya kamati ya Bunge la Kitaifa ya Uwekezaji wa Umma kuhusu Usimamizi na Elimu, inayoongozwa na Wamboka Wanami, kujibu ni kwa nini wamekatalia na kumiliki ardhi ya chuo cha RVIST.
Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Gideon Moi yamkini inamiliki ardhi hiyo kibinafsi.
Ardhi hiyo inaaminika kununuliwa mwaka 1972 na jamii ya eneo hilo kupitia kwa Harambee. Kisha Bodi ya Wakurugenzi iliteuliwa kusimamia chuo hicho ikiongozwa na Moi na inadaiwa haijarejesha ekari 5,000 ambazo chuo hicho kimejengwa.