Gavana Sakaja kuwalipa fidia wachuuzi

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja.

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amelaani vikali hatua ya askari wa baraza la jiji la Nairobi ya kuharibu na kutwaa toroli za wachuuzi siku ya Jumatano.

Askari hao waliharibu toroli za wachuuzi wa kuuza mayai na bidhaa zingine, hatua iliyowaghadhibisha Wakenya.

Kupitia mtandao wa X, Sakaja alisema serikali ya kaunti ya Nairobi imekuwa ikiwahimiza maafisa wake kuwahudumia wakazi wa jiji kwa uadilifu.

“Tumekuwa na uhusiano mwema na wachuuzi kwa muda wa mwaka mmoja, lakini katika siku za hizi maajuzi, kumekuwa na visa vinavyohujumu uhusiano huo. Tutachukua hatua za kinidhamu,”alisema Gavana Sakaja.

Aliamuru kuwa kila mchuuzi ambaye toroli yake iliharibiwa na askari wa baraza la jiji la Nairobi alipwe fidia ya shilingi elfu kumi kila mmoja.

“Hata ikiwa wachuuzi hao hawakuwa na stakabadhi husika, kama vile cheti cha afya kutoka kwa huduma ya afya ya umma ambacho ni lazima kumilikiwa na yeyote anayeshughulika na vyakula, hawangedhulumiwa kiasi hicho. Tunashughulikia swala hili,” aliongeza Gavana huyo.

Website |  + posts
Share This Article