Gavana Sakaja alifanyia mabadiliko Baraza lake la Mawaziri

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Nairobi Johnson sakaja.

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johson Sakaja, amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, mwaka mmoja tu baada ya kuchaguliwa afisini.

Kupitia kwa taarifa siku ya Alhamisi, Gavana huyo alisema mabadiliko hayo yalitekelezwa kuambatana na kifungu cha 31 (ba) (d) cha sheria ya serikali za kaunti ya mwaka 2012.

Katika mabadiliko hayo mapya, Maureen Njeri ambaye ni Waziri wa Mazingira, amehamishwa hadi wizara ya biashara.

Gavana huyo amempa Suzanne Silantoi jukumu la Waziri wa Afya na lishe, huku Rosemary Kariuki akijukumiwa Wzara ya Talanta, Ujuzi na Utunzi.

Dkt. Anastasia Nyalita ambaye alikuwa Waziri wa Afya, sasa atasimamia Wizara ya Ujumuishaji, Uhamasisho wa Umma na Huduma kwa Wateja.

Aidha Gavana Sakaja alimteua Brian Mulama kuwa Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi.

Waziri wa Fedha na Maswala ya Uchumi Charles Kerich atashikilia wadhifa huo sawia na Stephen Gathuita Mwangi ambaye ni Waziri wa Mipango ya Miji na Michael Magero Gumo ambaye ni Waziri wa Uvumbuzi na Uchumi wa Dijitali.

 

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *