Gavana Ochilo wa Migori asambaza mbegu kwa wakulima

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa Migori Dkt. Ochilo Ayako amezindua zoezi la usambazaji wa mbegu za thamani ya shilingi milioni 28 kwa wakulima wa kaunti hiyo.

Akizindua mpango huo katika eneo na Lichota kaunti ndogo ya Suna Magaribi, Ochilo amesema wakulima hao wana uwezo wa kumaliza njaa katika kaunti hiyo iwapo watapatiwa vifaa hitajika. Hivyo ameiomba serikali kuu kugatua majukumu na hela zote za kilimo.

Gavana pia ameongeza kuwa kaunti hiyo itapiga jeki wakulima 9,600 wa alizeti kwa kuwapa mbegu na mashine kwa lego la kuongeza usalishaji wa mafuta ya mmea huo katika wadi zote 40.

Katika zoezi hili, mbegu za mahindi, mahargwe, mchele na mtama zitasambazwa kwa wakulima 16,470 wamiliki wa mashamba ya jumla ya ekari 12,925.

Vile vile, maafisa 20 wa nyanjani wa kilimo na mifugo wameajiriwa ili kuboresha mpango huo.

Awamu ya pili ya zoezi hili itazinduliwa hivi karibuni ambapo wakulima 220 wamiliki wa mashamba ya jumla ya ekari 50 watanufaika katika eneo la Nyatike.

Share This Article