Gavana wa gatuzi la Meru Kawira Mwangaza amekamatwa na maafisa wa polisi.
Kulingana na ripoti, kiongozi huyo alikamatwa alipojaribu kuendeleza mpango wake wa Okolea katika eneo la Ruiga eneo bunge la Imenti ya kati.
Awali waziri wa mambo ya ndani Profesa Kithure Kindiki alikuwa amepiga marufuku mikutano yote ya mpango huo wa Gavana Mwangaza baada ya mojawapo ya mikutano hiyo kukumbwa na ghasia.
Mkutano wa leo pia unasemekana kukumbwa na ghasia.