Gavana wa kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka amezindua ujenzi wa soko la kisasa la kima cha shilingi milioni 343 eneo la Chwele.
Soko hilo likikamilika, litahudumia jumla ya wafanyabiashara zaidi ya 1,000.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Lusaka ametaja mradi huo kuwa utakaoinua uchumi wa eneo hilo husasan kwa wafanyabiashara wadogo na jamii ya eneo hilo kwa jumla.
Soko hilo litakuwa la pili kwa ukubwa nchini baada ya lile la Karatina.
Litakuwa na vibanda vya kuuzia bidhaa, majokofu, chumba cha mikutano, kituo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, afisi za kulipia ushuru, chumba cha kina mama na eneo la kuoshea bidhaa.