Gavana Guyo awahamisha mawaziri watano

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kauti ya Isiolo Abdi Hasaan Guyo amewahamisha mawaziri watano wa serikali yake kama njia ya kuimarsiha utendakazi.

Katika mabadiliko hayo ya Ijumaa, Salad Diba Rogicha alihamishwa kutoka wizara ya elimu ya chekechea na mifugo hadi ile ya barabara na usafiri, akimrithi Ali

Wario,ambaye sasa atasimamia wizara ya maji na usafi akichukua nafasi ya Godana Diba Abduba.

Kwenye uhamisho Godana amepelekwa katika wizara ya kilimo na unyunyuziaji, huku mtangulizi wake Salad Tutana,akihamishiwa wizara ya mafunzo ya kiufundi.

Stephen Kiambi, aliyekuwa katika wizara ya mafunzo ya kiufundi atasimamia elimu ya chekechea.

Serikali ya kaunti ya Isiolo ina mawaziri 31 walioidhinishwa na bunge la kaunti hiyo.

Share This Article