Gavana wa kaunti ya Migori Ochilo Ayacko, amekaribisha ziara ya Rais William Ruto katika kaunti hiyo, kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo.
Akizungumza na wanahabari afisini mwake, Ayako aliorodhesha maeneo ambayo alitaka yaangaziwe katika ziara hiyo, ambayo ni pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Lichota na kukamilishwa kwa ujenzi wa barabara.
Rais Ruto anatarajiwa kuzuru kaunti ya Migori leo Jumatano, huku akitarajiwa kuzindua mradi wa maji wa Kegonga,Kuria Mashariki, atakagua mradi wa unyunyizaji maji wa Kuja na kuzindua barabara ya Ngege-Mapera.
“TUnatarajia kuwa uzinduzi wa mradi wa unyunyiziaji maji wa Kuja, utapiga jeki shughuli za kilimo katika kaunti hii,” alisema Ayacko.