Gavana Achani aonya wamiliki wa ardhi kuzitumia au zitwaliwe na serikali

Marion Bosire
1 Min Read
Gavana wa Kwale Fatuma Achani.

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ametoa ilani kwa wamiliki wa ardhi wasiojulikana (Absentee Landlords) wamaomilki ardhi kubwa kuanza kuzitumia ardhi zao kimaendeleo la sivyo serikali yake itazichukua kufanyia mipango ya maendeleo.

Akizungumza katika eneo la Kinondo huko Msambweni,  Achani amesema kuna ardhi nyingi ambazo zinamilikiwa kinyume cha sheria katika fuo za bahari za kaunti ya Kwale hasa katika eneo la Diani na tayari serikali yake imeanzisha mchakato wa kuzirejesha kwa umma

Wakati huo huo Achani ameonya mabwanyenye wanaonyakua ardhi katika kaunti hiyo akisema atawakabili vilivyo na kudai kuwa serikali yake imekosa ardhi za miradi ya maendeleo kutokana na unyakuzi wa ardhi kwale.

Hata hivyo Achani amesema serikali yake imepiga hatua kubwa ya kukomboa ardhi za wakazi wa kwale akipigia mfano kurejeshwa kwa ardhi ya visiwa vya kisite Mpunguti na Chale kupitia tume ya maadili na kulambana na ufisadi nchini EACC na serikali yake.

Share This Article