Gavana Achani akabidhi boti kwa makundi ya wavuvi Kwale

Aidha, Achani amewakabidhi wavuvi kutoka makundi hayo manne vifaa vya uvuvi ikiwemo nyavu, mishipi, vifaa vya uokozi baharini, pamoja na vifaa vya kuhifadhi samaki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amekabidhi makundi manne ya uvuvi boti nne za kisasa za uvuvi pamoja na vifaa vya uvuvi eneo la Bodo huko Msambweni, kaunti ya Kwale.

Boti hizo zimekabidhiwa makundi ya uvuvi ya Malema, Mabaharia, Munje Bmu na lile Imani.

Hadi kufikia serrikali ya kaunti ya Kwale kupitia mradi wa KEMFSED unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, umekabidhi wavuvi katika ukanda wa kusini pwani zaidi ya boti 50 za kisasa za uvuvi na utalii katika mikakati ya kuzidisha pato la samaki kwa wakazi wa Kwale.

Aidha, Achani amewakabidhi wavuvi kutoka makundi hayo manne vifaa vya uvuvi ikiwemo nyavu, mishipi, vifaa vya uokozi baharini, pamoja na vifaa vya kuhifadhi samaki.

Akizingumza katika halfa ya kuwakabidhi wavuvi huko Bodo eneo la Ramisi, Gavana Achani amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuimarisha sekta ya uchumi samawati kupitia utoaji wa maboti ya kisasa na vifaa vya kisasa vya uvuvi ili kuimarisha na kutoa ajira kwa vijana wa Kwale.

Website |  + posts
Share This Article