Gavana Abdulswamad aongoza mpango wa kutoa damu

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, aliamua kuongoza kwa mfano pale alipojitolea kutoa damu kwenye mpango unaoendeshwa na wakfu wa Shariff Nassir, kampuni ya unga wa ‘Taifa’ na Shirika la RedSplash.

Kauli mbiu ya mpango huo wa kuchanga damu unaoendeshwa nje ya afisi ya Gavana Abdulswamad katika bustani ya Treasury Square mjini Mombasa ni “Upendo, Damu na Tabasamu”.

Abdulswamad alisema kwamba damu ni uhai na kiungo muhimu katika maisha ya mwanadamu, lakini uhaba wake mkubwa unahisiwa sio tu katika kaunti ya Mombasa bali kote nchini.

Anasema aliamua kuchanga damu kama njia ya kuwatia moyo wakazi wa Mombasa kujitokeza kwa wingi kusaidia.

Alikuwa ameandamana na mawaziri kadhaa wa serikali ya kaunti ya Mombasa akiwemo waziri wa barabara Dan Manyala, waziri wa biashara Mohammed Osman, waziri wa maji Emily Achieng, waziri wa utamaduni na jinsia Ken Ambani na Afisa mkuu mtendaji wa eneo la Swahilipot Mahmoud Noor miongoni mwa wengine.

Share This Article