Bingwa wa Afrika katika mbio za matembezi mwaka 2022 Samuel Gathimba Ireri na Sylvia Kemboi ndio washindi wa kilomita 10 matembezi katika siku ya kwanza ya mkondo wa pili wa mbio za AK zilizoandaliwa leo katika uwanja wa Thika.
Gathimba wa kutoka mkoa wa kati aliibuka bingwa kwa kutumia muda wa dakika 41 sekunde 44.7,akifuatwa na bingwa wa zamani wa dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 Heringstone Wanyonyi wa Kenya Police kwa dakika 42 sekunde 40.6 sna Stephen Ndangiri wa kdf katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Kemboi pia wa kutoka Central alishinda mbio za kilomita 10 wanawake alipotimka kwa dakika 49 sekunde 56.7,akifuatwa na Mercyline Nakhumicha wa Nairobi na Naum Jepkirui wa KDF katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Celestine Jepkosgei wa KDF ameshinda mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa wanawake akiziparakasa kwa dakika 10 sekunde 16.3,akifuatwa na mwenzake wa jeshi Dorothy Jepkoech Kimutai kwa dakika 11.00.04 na Ann Gathoni wa Police kwa dakika 11 sekunde 2.2 katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Mkondo huo wa pili utakamilika kesho