Gareth Southgate ajiuzulu baada ya kukamilika kwa Euro 2024

Tom Mathinji
1 Min Read
Gareth Southgate ajiuzulu wadhifa wa mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza.

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Uingereza Gareth Southgate, amejiuzulu siku chache baada ya timu yake kushindwa na Uhispania kwenye mechi ya fainali ya kombe la Euro 2024.

Katika fainali hiyo iliyochezwa Jumapili iliyopita Jijini Berlin Ujerumani, Uingereza ililazwa na uhispania mabao 2-1.

Ushinde huo ulikuwa wa pili mfululizo katika mechi ya fainali ya kombe la Euro, baada ya kuchapwa kupitia mikwaju ya penalti na Italia kwenye uwanja wa Wembley miaka mitatu iliyopita.

Southgate mwenye umri wa miaka 53, aliiongoza nchi yake katika mechi 102 ndani ya miaka minane akiwa kocha.

“Ni heshima kubwa katika maisha yangu kuichezea Uingereza na pia kuifunza timu ya uingereza,” alisema Southgate.

“Lakini sasa ni wakati wa mabadiliko na wa ukurasa mpya,” aliongeza mkufunzi huyo.

Mkataba wake ulikuwa unamalizika baadaye mwaka huu.

Mechi inayofuata ya Uingereza ni dhidi ya Jamhuri ya Ireland kwenye Ligi ya Mataifa tarehe 7 Septemba.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *