Gachagua: Serikali italipa bili za waathiriwa wa ajali ya Londiani

Tom Mathinji
1 Min Read

Naibu Rasi Rigathi Gachagua ametangaza kuwa serikali italipa bili za waathiriwa wa ajali ya Londiani.

Akizungumza alipoungana na viongozi na Wakenya katika eneo la Londiani kwa maombi ya madhehebu mbali mbali kufariji familia za waathiriwa wa ajali iliyotokea eneo hilo, Gachagua alisema msaada huo utakuwa ni pamoja na wa kifedha ili kufanikisha  shughuli za mazishi.

Alifariji familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, ambapo watu 52 walifariki.

Gachagua alitoa wito kwa wanaotumia barabara kuwa makini na kuahidi kwamba serikali itatumia kila mbinu kuhakikisha usalama barabarani.

Alitoa wito kwa serikali za kaunti kushirikiana na serikali ya kitaifa kubuni nafasi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ili kuepusha kuhatarisha maisha yao.

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen alisema wizara yake kupitia bunge la kitaifa itabuni sheria mpya zitakazojumuisha utumizi wa teknolojia kama vile kamera zitakazoonyesha kasi ya gari, mahali gari lipo na iwapo gari limekarabatiwa kama njia moja ya kupunguza ajali za barabarani.

Aliwasihi Wakenya kuendelea kusaidia familia za waathiriwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *