Gachagua: Mchakato wa kisiasa haupaswi kuvuruga amani na umoja

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Huku bunge likiendeleza mchakato wa kumbandua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani,  Gachagua ametoa wito kwa Wakenya kudumisha amani na umoja.

Gachagua amesema mchakato wa kisiasa haupaswi kusababisha taharuki hapa nchini.

“Natoa wito kwa Wakenya kudumisha amani na upendo miongoni mwao. Licha ya yale yanayoendelea, raia wa Kenya wanapaswa kuishi kwa amani, umoja na upendo,” alisema Gachagua.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika ukumbi wa maombi kwenye makazi yake rasmi mtaani Karen, Nairobi, Naibu huyo wa Rais alizitaka jamii zinazoishi katika eneo la Bonde la Ufa kuendelea kuishi kwa amani na utangamano na kuwaachia wanasiasa shughuli zao za kisiasa, akihimiza kwamba taifa ni muhimu kuliko kiongozi yeyote yule.

“Natoa wito kwa ndugu zetu wanaoishi eneo la Bonde la Ufa, kuwaachia wanasiasa mchakato huu. Watu wetu wanapswa kuanza kuishi pamoja na kuendelea na biashara zao,” alisihi Gachagua.

Aliongeza kuw Kenya ni taifa linaloendeshwa kwa misingi ya sheria na kueleza imani yake kwa mahakama katika jukumu lake la kulinda katiba na maamuzi ya raia.

Share This Article