Naibu Rais Rigathi Gachagua leo anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho ya kilimo na uwepo wa chakula cha kutosha nchini huko Bungoma.
Maonyesho hayo yameandaliwa na wizara ya kilimo na yanajiri kabla ya sherehe za siku kuu ya Madaraka ambazo zitaandaliwa katika kaunti ya Bungoma.
Maonyesho hayo ni ya wiki nzima Mei 27 hadi 31, 2024 huku sherehe za Madaraka zikiandaliwa Juni Mosi katika uwanja wa michezo wa Masinde Muliro mjini Bungoma.
Mawaziri Simon Chelugui wa vyama vya ushirika, Mithika Linturi wa Kilimo na Ufugaji na mwenzao wa Maji Alice Wahome watahudhuria maonyesho hayo katika chuo kikuu cha Kibabii.
Mada ya leo ya maonyesho hayo ni “Hatua za kuboresha upatikanaji na matumizi pembejeo za kilimo”.