Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema atafika mbele ya bunge la kitaifa kujitetea kesho saa kumi na moja jioni dhidi ya madaia ya ufisadi dhidi yake yanayolenga kumtimua afisini.
Gachagua amesema hakuna sababu zozote za kumtimua afisini akitaka familia yake kutohusishwa katika sakata na madai yanayolenga kumng’atua afisini kesho.
Naibu Rais akihutubia taifa amesema madai yote dhidi yake ni hujuma na kuwatesa watoto wake ambao wameekeza kwenye biashara mbalimbali.
Gachagua ameapa kuwaabishia waliowasilisha kesi hiyo kesho atakapofika bungeni kujitetea.
Gachagua amekana kuhusika katika zabuni ya vyandarua vya mbu ya thamani ya shilingi bilioni 3.7 na kusema kuwa kampuni ya mwanawe haikufanikiwa kupewa zabuni.
Gachagua amesema hakuna ushahidi wa yeye kushawishi kuhusu zabuni hiyo na wala kamwe kampuni ya mwanawe haikupewa zabuni.