Bunge la Senate Alhamisi usiku, limemvua Rigathi Gachagua wadhifa wa Naibu Rais.
Hatua hiyo ilijiri baada ya kupatikana na makosa matano kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake.
Gachagua amevuliwa wadhifa huo huku akiwa amelazwa hospitalini, akisemekana kuwa na maumivu ya kifua.
Maseneta walipigia kura kila shtaka dhidi ya Gachagua, katika kikao hicho cha Alhamisi alasiri.
Gachagua sasa anakuwa Naibu Rais wa kwanza hapa nchini kubanduliwa wadhifani, chini ya katiba ya mwaka 2010.
Baadhi ya makosa ambayo yalimkabili Gachagua ni pamoja na ukiukaji wa katiba, kupata mali kwa njia isiyo halali, kumshambulia Jaji wa Mahakama, ukabila, kutomtii Rais na kudhalilisha ugatuzi miongoni mwa maswala mengine.