Mageuzi ya sekta ya majani chai: Gachagua ataka kesi ziondolewe kortini

Martin Mwanje & DPCS
1 Min Read

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito wa kuondolewa mahakamani kwa kesi zinazotatiza utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya majani chai.

Amesema kesi hizo zinazuia wakulima kupata mapato ya juu kutokana na zao hilo.

Naibu Rais amesema si vyema kwa wadau katika sekta hiyo kuwasilisha kesi mahakamani zinazozuia juhudi za kuifanya sekta hiyo kuwavutia zaidi wakulima wanaostahili kupata mapato bora.

“Kesi zinazowasilishwa mahakamani zimezuia utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya majani chai. Natoa wito kwa wadau ambao wana nia njema kuondoa kesi hizo na kuruhusu mageuzi haya kutekelezwa kikamilifu kwa manufaa ya wakulima,” alisema Gachagua.

Aliyasema hayo leo Alhamisi alipoongoza hafla ya utoaji ripoti ya utendakazi wa sekta ya majani chai ya mwaka 2023.

Ripoti hiyo ilitolewa na Bodi ya Majani Chai ya Kenya katika jumba la majani chai jijini Nairobi.

Martin Mwanje & DPCS
+ posts
Share This Article