Gachagua aondolewa katika wadhifa wa naibu kiongozi wa chama cha UDA

Marion Bosire
1 Min Read
Rigathi Gachagua.

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ameondolewa kwenye wadhifa wa naibu mwenyekiti wa chama tawala UDA, na mahala pake kuchukuliwa na naibu rais Kithure Kindiki.

Katika taarifa, kamati kuu cha kitaifa ya chama cha UDA ilisema kwamba ilikita uamuzi wake katika maamuzi ya bunge la taifa na bunge la Seneti wa kumbandua afisini kama naibu rais.

Naibu Rais Kindiki anaanza kuhudumu katika wadhifa huo mara moja kulingana na taarifa iliyotiwa saini na mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha UDA Cecily Mbarire na naibu mwenyekiti wa kitaifa Hassan Omar.

Mbarire na Omar katika taarifa hiyo waliorodhesha vifungu vya katiba ya Kenya na vya katiba ya chama cha UDA vinavyowezesha uamuzi huo wa leo.

“Mheshimiwa Rigathi Gachagua hawezi kutekeleza majukumu ya afisi ya Naibu Kiongozi wa Chama na hivyo anakoma kushikilia wadhifa wa Naibu Kiongozi wa Chama.” ilisema taarifa hiyo ya Novemba 11, 2024.

Share This Article