Naibu Rais aliyeng’atuliwa mamlakani Rigathi Gachagua amelazimika kukimbilia usalama, baada ya wahuni kumshambulia alipokuwa kwenye mazishi eneo la Limuru kaunti ya Kiambu siku ya Alhamisi.
Gachagua alikuwa akihudhuria mazishi wakati genge la wahuni lilipovamia hema alipokuwa ameketi wakimpura kwa mawe na hata kupasua madirisha ya gari lake.
Iliwabidi walinzi wake kujitahidi na kufanikiwa kumtorosha, huku mali ya thamani isiyojulikana ikiharibiwa.
Vurumai zilizuka wakati mbunge wa zamani wa Limuru Peter Mwathi, aliposimama kuwahutubia waombolezaji.
Kisa hicho kimejiri siku chache baada ya Gachagua kukiri kuwa kuwa watu wasiojulikana ambao wamekuwa wakimwandama kila mahali kwa lengo lisilojulikana.