Gachagua akanusha mashtaka dhidi yake akisema ni porojo

Dismas Otuke
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, ameweka paruwanja chanzo cha mali yake anayomiliki na kukanusha madai kuwa yeye ni mfisadi.

Gachagua aliyasema hayo Jumatatu usiku, saa chache kabla kufika mbele bunge kujitetea dhidi ya kutimuliwa kwake afisini.

Akihutubia taifa kutoka afisini mwake Jumatatu jioni, naibu huyo wa Rais, alisema nyingi ya mali anayomiliki inayodaiwa ya ufisadi ni urithi wa mali ya marehemu ndugu yake Nderitu Gachagua.

“Baadhi ya mali ambayo yametajwa na mbunge Mutuse Mwengi katika hoja ya kuniondoa mamlakani, kama vile hoteli ya Olive Garden na Queens Gate Apartment, ni miongoni mwa mali niliyorithi kutoka kwa ndugu yangu,” alisema Gachagua.

Alisema yuko tayari kufika mbele ya  ya bunge la kitaifa kesho Jumanne saa kumi na moja jioni, kujitetea dhidi ya tuhuma hizo akisisitiza kuwa hoja ya kumbandua afisini haina msingi wowote.

Share This Article