Waziri Mkuu mpya wa muda nchini Gabon Raymond Ndong Sima ametangaza kuwa uchaguzi mkuu huenda ukaandaliwa baada ya miaka miwili.
Sima aliyeshika hatamu Alhamisi wiki hii wiki moja tu baada ya kuapishwa kwa Rais wa Kijeshi Jenerali Brice Nguema kufuatia mapinduzi ya jeshi yaliyomngátua mamlakani Rais Ali Bongo .
Raia nchini Gabon walifurahia mapinduzi hayo yaliyotokea siku moja tu baada ya matokeo ya uchgauzi mkuu yaliyomtangaza Bongo kuhifadhi kiti chake.
Waziri mkuu huyo mpya ambaye alishindwa na Bongo katika chaguzi mbili zilizopita akikataa kuwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya Urais.
Bongo aliachiliwa huru kutoka kifungo cha nyumbani siku ya Alhamisi ili kupokea matibabu barani ulaya.