Freddie Leonard azomea wanablogu wanaofuatilia ndoa yake

Mwigizaji huyo amekasirishwa na wanablogu ambao wanawafuatilia sana na kukisia mambo yasiyo na ukweli wowote.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nigeria au ukipenda Nollywood Freddie Leonard amezomea wanablogu ambao anasema wanafuatilia ndoa yake na mwigizaji mwenza Peggy Ovire.

Katika taarifa aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Leonard aliwataja watu hao kuwa wasiokuwa na la kufanya na wanaonusanusa ndoa yao kama mbwa.

Alisema yeye na mke wake hawana jukumu la kujieleza kwa yeyote akisema kwamba Peggy sio mfungwa katika ndoa na kwamba anaweza kufanya lolote apendalo.

Freddie alimtetea mkewe kwa kuchapisha picha za Krismasi bila yeye na kuonekana kwenye picha bila pete ya ndoa.

“Mimi ndio nilinunua pete hiyo na silalamiki asipoivaa.” aliandika Leonard.

Mwigizaji huyo alitaja mitandao ya kijamii kuwa yenye sumu sikuhizi akishangazwa na jinsi watu wanajitolea kufuatilia wengine.

Alifafanua kwamba hatabadili kazi yake ya uigizaji kufurahisha watu akitaja hasa majukumu ya uigizaji ambapo anahitajika kuonyesha mapenzi kwa kupigana mabusu na waigizaji wengine.

“Sitaacha kupigana mabusu kwenye uigizaji kwa sababu sasa niko kwenye ndoa, au kwa sababu ya vile watu wengine wasio na ufahamu watanichukulia.” alifoka Leonard.

Leonard alimalizia kwa kusema, “Mimi na Peggy hatukuwauliza wakati tulioana na hivyo hatuwajibiki kwenu.”

Ndoa ya Freddie na Peggy imekuwa ikiangaziwa sana mitandaonina hatua ya Leonard ya kuzomea wakosoaji inaonekana kuwa ya kujaribu kukomesha wanaowaangazia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *