Francis Gaitho kujiwasilisha kwa DCI

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamitandao Francis Gaitho amesema kwamba atajiwasilisha kwenye afisi za idara ya upelelezi wa jinai DCI katika jumba la Mazingira leo,wakati wowote kuanzia sasa.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, Gaitho ameelezea kwamba atafika huko saa nane alasiri huku akishukuru wote ambao walikuwa wanahofia usalama wake.

Alielezea pia kwamba anawasiliana na wakili wake na anajua cha kufanya.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya maafisa wa polisi kumkamata mwanahabari mkongwe Macharia Gaitho na kisha kumwachilia huru na kuelezea kwamba walimkamata kimakosa kwa kumdhania kuwa Francis Gaitho.

Huduma ya Taifa ya Polisi NPS ilitumia mtandao wa X kuelezea hayo ikifafanua kwamba haiwalengi wanahabari kwa njia yoyote.

Binti ya Macharia Gaitho kwa jina Anita Gaitho ndiye alitangaza kile alichokitaja kuwa kutekwa nyara kwa babake na watu waliokuwa wakiendesha gari aina ya Probox nambari ya usajili KBC 725J.

Anita alielezea pia kwamba babake alipelekwa katika kituo cha polisi cha Karen ambako aliachiliwa na kwamba alidhulumiwa wakati wa kisa hicho.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *