Chama cha Ford Kenya chake Spika wa Bunge la kitaifa, Moses Wetangula siku ya Jumapili kimewapokea wanachama waliokihama chama cha Orange Democratic Movement – ODM.
Katibu Mkuu wa Ford Kenya ambaye pia ni mbunge wa Tongaren Milicent Abudho, ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa kitaifa wa chama, amewapokea wanachama hao wapya akisitiza azima ya chama hicho kuwasajili wanachama wapya zaidi kote nchini.
Hafla hiyo imeandaliwa nyumbani kwa katibu mratibiu wa chama hicho katika kijiji cha Namuduru, eneo la bunge Funyula.