FKF yazindua bodi ya uchaguzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Kandanda nchini Kenya, FKF limezindua bodi ya wanachama watano itakayosimamia uchaguzi wa mwaka huu.

Bodi hiyo itaongozwa na mwenyekiti Hesbon Owilla huku Merceline Sande akiwa katibu.

Wanachama wengine ni Kinara wa Chama cha Wanahabari wa Michezo nchini Kenya (SJAK), Mwenyekiti wa zamani wa AFC Leopards Dan Mule na Alfred Ng’ang’a .

Bodi hiyo inajukumiwa na kutoa mpangilio wa uchaguzi na kuhakikisha utakuwa huru na wa haki.

Uchaguzi wa FKF umeratibiwa kuandaliwa kabla ya Disemba 15 mwaka huu huku mwenyekiti wa sasa Nick Mwendwa akiwania muhula wa tatu.

Share This Article