Shirikisho la kandanda nchini FKF limeanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma za upangaji matokeo zinazomhusisha kipa wa Harambee Stars na klabu ya Kakamega Homeboyz, Patrick Matasi.
Haya yanajiri baada ya kuzagaa mitandaoni kwa video zinazomhusisha Matasi akishiriki mazungumzo ya kupanga matokeo ya mechi na mtu asiyejulikana.
FKF imewataka wananchi walio na taarifa kuhusu kashfa za mchezaji huyo kupanga matokeo ya mechi kuwasilisha kupitia kwa barua pepe .