FKE yahofia asilimia 40 kupoteza ajira kutokana na makali ya ushuru

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Waajiri nchini FKE linahofia kuwa asilimia 40 ya watu  nchini Kenya,huenda wakapoteza kazi zao endapo serikli haitarekebisha matozo mapya ya ushuru yaliyoanza kutekelezwa.

FKE kwenye kikao na wanabari wanahoji kuwa ushuru mpya ulioanza kutekelezwa kuanzia Julai kwenye sheria za fedha za mwaka 2023 , ukiwemo ule wa nyumba,ushuru wa thamani ya bidhaa VAT kwa mafuta na matozo mapya ya afya yameongeza gharama kwa waajiri .

FKE inasema endapo sheria hizo za ushuru hazitarekebishwa waajiri wengi watalazimika kuwachuja wafanyikazi kadhaa ili kupunguza gharama.

Kulingana na utafiti  zaidi ya waajiriwa 70,000 wamesimamishwa kazi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kutokana na kuongezeka kwa gharama ya mashirika na kampuni mbalimbali hali iliyochangiwa na mfumuko wa bei za bidhaa.

Share This Article