Shirikisho la Soka Duniani FIFA limezindua mpira rasmi wa Trionda utakaotumika katika mechi za fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao kwa pamoja na mataifa ya Canada, Mexico na Marekani.
Hafla hii imeandaliwa mapema leo Ijumaa zikiwa zimesalia siku 250, kabla ya kungóa nanga kwa kindumbwendumbwe hicho kitakachoshirikisha mataifa 48 kwa mara ya kwanza.
Mpira huo una rangi tatu za kijani, nyekundu na samawati zinazoashiria mataifa matatu yatakayoandaa kipute hicho.

Droo ya Makala ya 23 ya Kombe la Dunia imeratibiwa kuaandaliwa mjini Washington, Marekani, Disemba 5 mwaka huu.