FIFA yazindua mpira rasmi utakaotumika kwa nusu fainali na fainali ya Kombe la Dunia

Robo fainali zitakamilika  Jumapili hii Julai 12, kabla ya nusu fainali kachezwa baina ya Julai 14 na 15.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limezindua mpira mahususi utakaotumika kwa mechi za nusu fainali na fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu.

Mpira huo aina ya Trionda ni tofauti na ile ya awali ambayo itatumika hadi kufikia robo fainali kwani ina rangi ya dhahabu.

Mpira wa Trionda ambao umekuwa ukitumika unajumuisha rangi nyekundu, samawati, kijani na nyeupe.

Robo fainali zitakamilika Jumapili hii, Julai 12 kabla ya nusu fainali kachezwa baina ya Julai 14 na 15.

Fainali itakasatwa Julai 19 ugani New York/New Jersey.

 

Share This Article