FEASSSA 2024: Musingu kuchuana na Kitende nusu fainali

Tom Mathinji
2 Min Read
Mashindano ya shule za upili za Afrika Mashariki zinaendelea nchini Uganda.

Shule ya wavulana ya Musingu, itakabana koo kesho Jumapili na St. Mary’s Kitende ya Uganda katika nusu fainali ya soka ya kipute cha shule za upili za Afrika Mashariki kinachoendelea mjini Mbale, nchini Uganda.

Hii ni baada ya timu hiyo kuibuka ya pili katika kundi B kwa alama nane, nayo Kitende ikaongoza kundi A kwa alama 10.

Nusu fainali ya pili ni kati ya wenyeji Bukedea Comprensive school na Amus college.

Waakilishi wengine wa Kenya (Highway na St.Joseph), walibanduliwa kwenye awamu ya makundi haswa walipolazwa leo Jumamosi na Bukedea na Kitende bao moja na magoli matatu kwa nunge mtawalia.

Kwenye nusu fainali ya voliboli, akina dada wa Kesogon watakabana na St. Elizabeth (UG) baada ya kuwazidi nguvu Masasi (TZ) seti tatu kwa yai za 25:16, 25;13 na 25:13. Kwanzanze watachuana na Bukedea.

Katika nusu fainali ya mogongo, Musingu iliilemea St.Antony (KE) mabao mawili kwa moja nayo St.Charles (KE) ikawaadhibu Ntare (UG) matuta mawili kwa sufuri baada ya sare ya magoli mawili kwa mawili katika muda wa kawaida. Washindi hao watachua kwenye fainali ya hapo kesho.

Vile vile, timu za Kenya ziliandikisha matokeo mseto kwa mchezo wa vikapu. Akina dada wa St.Joseph walivuna ushindi wa alama 17 dhidi ya tisa ya APE Rugunga (RW).

Butere walilazwa na St.Noa(UG) alama 14 kwa 5 nayo Kitende (UG) ikaishinda Nasokol alama 19 kwa tano.Pia Raila Education Centre ilikwatuliwa alama 17 kwa sita na Seroma (UG).

Share This Article