Fataki ya  Ogam yaipa Harambee Stars ushindi dhidi ya Burundi

Dismas Otuke
1 Min Read

Bao la dakika ya 73  lake Ryan Ogam liliipa Kenya ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wenyeji Burundi, katika mechi ya kundi F ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao  iliyopigwa Alhamisi jioni uwanjani Intwari.

Ushindi huo umeipelekeza Harambee Stars hadi nafasi ya tatu kundini humo kwa alama 12.

Kenya, inayonolewa na kocha Benni McCarthy, itakamilisha mechi zake za kufuzu Jumanne ijayo dhidi ya Ivory Coast mjini Abidjan.

Tembo wa Ivory Coast ambo pia ni mabingwa wa wananusia kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao wakiongoza kwa alama 20,moja zaidi ya Gabon iliyo ya pili.

Website |  + posts
Share This Article