Familia yaghubikwa na majonzi baada ya ugomvi wa watoto kuishia mauti

Marehemu ambaye ni msichana wa umri wa miaka 16 mkazi wa eneo la Fanaka Narok ya kati alipoteza maisha baada ya kuvuja damu nyingi kutoka kwenye jeraha la kisu alilosababishiwa na binamu yake.

Marion Bosire
1 Min Read

Ugomvi kati ya watoto wawili ambao ni mabinamu uliishia katika kifo cha mmoja baada yake kudungwa kisu katika kisa kilichoripotiwa kwenye kituo cha pilisi cha Narok jana.

Marehemu ambaye ni msichana wa umri wa miaka 16 mkazi wa eneo la Fanaka Narok ya kati alipoteza maisha baada ya kuvuja damu nyingi kutoka kwenye jeraha la kisu.

Alisababishiwa jeraha hilo na binamu yake ambaye pia ni msichana wa umri wa miaka 17 baada yao kugombana.

Majirani ambao hawakutarajia tukio hilo walijaribu kuingilia kati kutuliza ugomvi lakini walikuwa wameshachelewa na hawakuweza kuokoa maisha ya mwathiriwa aliyethibitishwa kufariki punde alipofikishwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Narok.

Msichana aliyetekeleza mauaji hayo amekamatwa na polisi na atafikishwa mahakamani Jumatatu Disemba 23, 2024, huku polisi wakichunguza kilichosababisha ugomvi kati ya mabinamu hao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *