Familia ya kocha wa Kiptum yakataa matokeo ya upasuaji yataka uchunguzi kubaini chanzo cha kifo

Dismas Otuke
1 Min Read

Familia ya kocha wa aliyekuwa mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum  imekataa matokeo ya upasuaji wa mwili wa Gervais Hakizamana, aliyefariki pamoja na mwanariadha huyo katika ajali ya barabarani wiki iliyopita katika barabara ya Kaptagat.

Familia hiyo kupitia kwa mpwa wa marehemu kocha Sandrine Hakizimana, inahoji ripoti ya upasuaji uliofanywa na Paholojia wa serikali Benson Macharia, iliyoashiria kuwa kocha huyo alifariki kutokana na majeraha ya kichwani na shingoni wakisema kuwa walipotazama mwili wa marehemu haukuwa na majeraha ya kichwani wala shingoni.

Familia hiyo badala yake imetaka uchunguzi wa kina kufanyika kubaini kiini halisi cha vifo vya Kiptum na kocha huyo.

Mwili wa kocha huyo umesafirishwa kwa ndege hadi nchini Rwanda mapema Jumamosi ambapo utalazwa katika makafani ya Hostpitali ya Polisi ya Kacyiru, kabla ya kusafirishwa hadi Masaka,wilayani  Kicukiro kabla ya mazishi ya Februari 21 .

Website |  + posts
Share This Article