Serikali imehamisha familia 50 zinazoathirika na mafuriko katika kaunti ndogo ya Limuru kaunt ya Kiambu, kufuatia mvcua kubwa inayoshuhudiwa kote nchini.
Familia kumi kati ya zile zilihamishwa zilikuwa zikiishi karibu na kinamasi cha Manguo eneo la Limuru huku nyingine 40 zikiishi katika maeneo ya Kwambira, Kamirithu, Farmers na Karanjee.
Mvua kubwa inayoshohudiwa nchini imesababisha maafa na hasara kubwa katika maeneo mbalimbali nchini tangu mwanzoni mwa mwezi huu.