Familia 50 zaachwa bila makao Kiambu kufuatia mkasa wa moto

Marion Bosire
1 Min Read

Mali ya thamani isiyojulikana imeharibiwa na familia 50 kuachwa bila makao baada ya moto kuteketeza nyumba zao usiku wa manane katika kijiji cha Farmers eneo bunge la Limuru kaunti ya Kiambu.

Majirani ambao walijaribu kusaidia kuzima moto huo walielezea kwamba ulianzia kwenye nyumba moja na kusambaa hadi kwenye nyumba zingine lakini chanzo bado hakijabainika.

Wanaomba serikali kuu na serikali za kaunti kuanzisha hazina za kusimamia mikasa kama hiyo ambazo zitasaidia wanabiashara na wakazi kujijenga upya.

Waathiriwa wanaomba msaada wa mavazi na mahitaji mengine ya msingi kama vitabu na sare za shule ndiposa hata watoto waweze kuendelea kuhudhuria masomo shuleni.

Share This Article